Church

Efatha Ministry Hai Kilimanjaro

Bomang'ombe, 1058 Moshi

About

Huduma ya Uponyaji & Ukombozi kwa Damu ya Yesu Kristo

Tags : #ReligiousCenter, #ChristianChurch, #ReligiousOrganization

Location :
Bomang'ombe, 1058 Moshi

19 Reviews

  • Anynomous
    26 August 2018

    Somo. MAOMBI YA MLIMA KARMELI. Maombi ya mlima karmeli ni maombi ya kubadilisha mawazo ya kusitasita. Kila mtu aliye hai na anaishi analo kusudi la kutimiza hapa duniani. Umeumbwa kwa kusudi la Mungu nalo lipo ndani yako, ili ufikie kusudi lako unapaswa kutambua majira na nyakati. Kusudi lako limebeba mafanikio yako . Mafanikio yanakwenda na majira na nyakati. Huwezi kufanikiwa kama haufahamu kusudi lako, kusudi lako ndilo linalokupa aina ya maombi ya kupeleka mbele... za Mungu.

    Mhubiri 3:1–8 Hakuna jambo ambalo halipo kwenye majira na nyakati. Shughuli za kibinadamu zitakuwa na maumivu na uchungu kama hutojua majira na nyakati.

    Mhubiri 3:9–13 Kama hutojua wakati hutoona faida ya unachotenda na utapata taabu na kutaabika na kushindwa kuelewa kitu kizuri alichokiweka (Mungu) ndani ya moyo wako yaani kusudi. Haulitafuti kusudi unalo bali tafuta majira na wakati wa kutimiza maana unapopoteza muda unachelewesha kusudi lako kutimia. Hutoweza kuivumbua kazi ya Mungu ndani yako kama hujui majira na nyakati, wala hutoburudisha mwili wako kwa kula vizuri na kunywa kama hutojua majira na nyakati.

    Mathayo 5:14 Wakati husababisha nuru yako kuangaza, na majira ndiyo yanakupa kuwa na ladha ya Mginguni. ~Kwenye majira kuna mambo mawili:- (1) Kujiandaa na kuwa tayari (2) Kudhamiria. Muda na wakati ndio utakaokupa muelekeo wa kulitimiza kusudi lako.

    See More

    report this review
  • Anynomous
    26 August 2018

    Yesu nakuita Yesu asubui ya leo nataka nikuone Yesu

    report this review
  • Anynomous
    20 August 2018

    MT. JOSEPHAT LEMA. Isaya 40:1–4 Tuliza moyo maana Bwana atakuja kwa wote wenye mwili na utukufu wake utauona. Mtengenezee Bwana njia ili apate kutimiza mapenzi ya Mungu kwako.

    Ezekiel 18:28–30... Njia ni muelekeo, mtengenezee Bwana mwelekeo wako. Chochote ulichoshindwa kufikia kina chanzo, ondoa chanzo cha tatizo ili uweze kufaulu. Tabia za kujirudia hukufanya ushindwe kumtengenezea Bwana njia. Maumivu yana tabia ya kujirudia, ili usikutane na maumivu mtengenezee Bwana njia.

    Hosea 2:14 Kaa hapohapo jangwani maana Bwana atasema nawe na kukutuliza moyo.

    MASIHI NA NYAKATI ZAKE. Masihi ni mpakwa mafuta wa Mungu. Kuadhibiwa na Mungu sio mwisho, kupitia kwenye adhabu sio neno la mwisho la Mungu. Amekusudia kutimiza ahadi zake kwangu ingawa namuasi mara kwa mara.

    Isaya 4:3–4 Mungu hataki taifa / mtu aangamie bila kutimiza aliyo kusudia. Nyakati za Bwana zinakuja zitakuwa na heri. Itakuwa ni nyakati za kurudishiwa kile kilicho potea na hakutakuwa na laana tena. Nyakati za masihi ni za kukusanya na sio kutawanya.

    Isaya 30:25–26 Amekusudia ardhi kuzama na taifa / watu wake kutwaa kisasi juu ya adui zao.

    Mika 4:11–13 Kipindi chako kimefika na pembe yako imeota kwakuwa unatembea na Bwana, na adui zako utawaponda.

    See More

    report this review
  • Anynomous
    19 August 2018

    Twakupenda, Twakuabudu, Hallelujah hakuna kama wewe Bwana.

    report this review
  • Anynomous
    19 August 2018

    Unastahili kuabudiwa na hakuna kama wewe Mungu wetu.

    report this review
  • Anynomous
    12 August 2018

    MCH. LOSERIAN MOLLEL ENENDENI KWA ROHO NDIPO MTAWEZA KUZISHINDA TAMAA ZA MWILI. Ufunuo 21:1–8 Ukaapo hapa duniani tazamia mbingu mpya na nchi mpya. Angalia sana usije naswa na dunia hii maana kila kitu kitapita na mambo yote yatapita. Waliokubali kusulubisha miili yao ndio watakao ingia mbingu mpya na nchi mpya ambayo haina machafuko ya dunia hii. Maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu kwa wale walio tayari na walio achana na mambo ya dunia hii.

    ...

    2Wakorintho 5:17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. Unapokuwa umefanywa upya na umekuwa kiumbe kipya ya kale usitamani wala kuyafanya tena.

    Isaya 43:18–19 Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na mito ya maji nyikani. Achana na mambo ya kale na tabia za kale maana kuna jambo jipya katika nchi mpya ambayo Bwana amekuandalia. Kwa anayetazamia mbingu na nchi mpya hana mashaka, wasiwasi, woga wala hofu ndani yako maana Bwana atakupa chemchemi ya maji ya uzima. Unapokuwa mwana wa Mungu kuna vitu utavirithi kutoka kwake na utakuwa mwanae.

    Ufunuo 21:9–27 Kwa aliyeamini anapewa vitu vya kuona na kuonyeshwa mji mtakatifu ( Yerusalem ). Yeyote aliye nunuliwa na kuokolewa kwa damu ya mwana kondoo atapewa kuingia katika mji mtakatifu uliopambwa kwa dhahabu na lulu. Katika mji na nchi mpya hakitaingia kinyonge wala afanyae machukizo mbele za Mungu.

    See More

    report this review
  • Anynomous
    12 August 2018

    Niguse tena, nakuomba Bwana uniguse tena. Amen!

    report this review
  • Anynomous
    12 August 2018

    USHUHUDA. Alikuwa na uvimbe tumboni na baada ya kuombewa na Mch. Loserian kapokea uponyaji wake. Karudi Mwimbili kupima uvimbe hakuna. Jina la Bwana litukuzwe. Amen!

    report this review
  • Anynomous
    12 August 2018

    Eeh Yesu nakuinulia macho yangu, maisha yangu, nikitazama na afya niliyo nayo nakutukuza. Baba kwako ninaweka kila kitu nasema niwewe tuu unastahili kuinuliwa asubui yaleo.

    report this review
  • Anynomous
    30 July 2018

    MCHUNGAJI. LOSERIANI MOLLEL SOMO: ENENDA KWA ROHO NDIPO UTAWEZA KUSHINDA TAMAA ZA MWILI. Wagalatia 5:16–26 Unapookoka unaruhusu Roho Mtakatifu akuongoze katika maisha yako. Mwili ni udongo kadri unavyozidi kukua kuna tabia huchipua, kwahiyo mpe Yesu nafasi ili aponde ponde na kuua zile roho na tabia zinazo chipua. Roho anakuongoza katika mambo mema na mafanikio. Mwili na Roho hushindana ndani ya mtu mmoja na haiwezekani wote wawe sawa. Ukiwa mtu wa mwilini sana Roho ...huondoka ila ukiwa mtu wa rohoni, Roho huchukua nafasi katika maisha yako. Ukiishi kwa Roho inakupasa uenende katika Roho na sio mwili. Walio wa Kristo wamesulubisha mwili msalabani pamoja na tamaa zake. #ONYO Kama unataka kuishi katika mwili unataka kufa kifo cha sasa na chabaadaye, bali kama unataka kuishi ishi katika Roho. Warumi 8:1–17 Kuna mambo ukimsikiliza Roho unafikia mafanikio yako kwa haraka. Lolote unalotenda ambalo umeongozwa katika Roho hutojutia maana hakuna adhabu. Yesu alikuja kuhukumu dhambi ya mwili. Ukifikiria mambo ya mwili utayafuata na kutenda hayo bali ukifikiria na kujishughulisha na ya Rohoni utafuata na kutenda yaliyo ya Rohoni. Nia ni ya mwilini ni mauti bali nia ya Roho ni uzima wa milele na amani. Mwili hauwezi kumpendeza Mungu kwakuwa hautii sheria zake.

    See More

    report this review
  • Anynomous
    29 July 2018

    Ni wewe Mungu pekee unayestahili kuabudiwa, kuheshimiwa na kupewa sifa. Hakuna mwingine anayestahili wala wa kulinganishwa na wewe wala wa kufananishwa na wewe. Tunakuabudu Mungu wetu.

    report this review
  • Anynomous
    22 July 2018

    MTUMISHI JOSEPHAT LEMA SOMO: TUMAINI LANGU NI NANGA YANGU. TUMAINI ni kiwango cha juu cha Imani. Kama hauna tumaini kwa Mungu usitarajie kitu chochote kutoka kwake. Kuna mambo ameweka mbele yangu na hayo ndiyo ninayatarajia kuyapokea kwakuwa namtumaini. Waebrania 6:18–20

    ...Continue Reading

    report this review
  • Anynomous
    22 July 2018

    Mtakatifu ni wewe Mungu wetu na hakuna aliye kama wewe. Tunaungana na maserafi na makerubu tukisema hakuna aliye kama wewe.

    report this review
  • Anynomous
    09 July 2018

    Matukio. Hongera sana Joshua kavishe na Schola Buai. Mungu akawe pamoja nanyi katika maisha yenu.

    report this review
  • Anynomous
    11 June 2018

    MT. JOSEPHAT LEMA. KUNA MAHALI UNASUBIRIWA ILI VITU VITOKEE. Kuna mahali unasubiriwa ili vitu vitokee na kama hutokwenda hapo hakuna kitu kitakacho tokea.

    Mwanzo 2:4–5 Hivyo ndivyo vizazi vya mbingu na nchi zilipoumbwa. Siku ile BWANA Mungu alipoziumba mbingu na nchi hapakuwa hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado kwa maana BWANA Mungu hajainyeshea nchi mvua wala wala hapana mtu wa kuilima ardhi.... Wala Mungu hawezi kuleta mvua hapo kwa kuwa hujaonekana. Kazi ya Mungu ni kuleta mvua na kazi yako ni kusababisha vitu vitokee.

    Mwanzo 1:26 Mungu akasema na tufanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; wakatawale samaki wa baharini na ndege wa angani, na wanyama na nchi yote pia na kile chenye kutambaa kitambaacho juu ya nchi. Kuna mambo mawili hapa i/ Sura ya Mungu ii/ Mfano wa Mungu Sura ni muonekano halisi na Mfano ni utawala au umiliki. Kila ninapo kuwepo ninamwakilisha Mungu kwa kuwa nina sura na mfano wake.

    Kuna kitu kimeingilia mawasiliano yako na Mungu. Marko 7:21–22 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivu, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Moyo wako umekuwa na mahusiano na mambo mengine na ndio maana umepoteza mahusiano na mawasiliano mazuri na Mungu. Umekuwa na mahusiano na yale mambo unayowasiliana nayo na umeishi katika hayo na kuharibu mahusiano yako na Mungu. Umekwenda katika tafsiri na moyo wako umekosa kuishi katika uhalisi, kwahiyo maisha yako unaiga kwa mataifa badala ya kuishi kwenye uhalisi.

    Waefeso 4:17–24 Mungu hajakuumba uishi hivyo unavyo ishi, unaishi kwa kutegemea akili zako na kutegemea hisia za mwili na ndani ya maisha yako umejaza utu wa nje, tafsiri na mwonekano wa nje. Unaishi katika akili zako za kawaida na ndizo zinazoongoza mwenendo wako. Unafanya maamuzi kutokana na muonekano wa nje na hilo sio kusudi la Mungu kuumba Roho zetu, alitaka maamuzi yako yaamuliwe na Roho na sio akili, nafsi, au muonekano. ISHI KWA MUONEKANO WA NDANI.

    See More

    report this review
  • Anynomous
    10 June 2018

    Ni wew Mungu pekee wastahili kuabudiwa

    report this review
  • Anynomous
    04 June 2018

    KUJIBIWA MAOMBI UNAPATA NGUVU YA KUENDELEA MBELE. Ester 9:11–32 Kitendo cha kujibiwa maombo unapata nguvu ya kuendelea mbele katika mapambano yako ya kivita. Unapopata nguvu usimzime Roho Mtakatifu ruhusu tena atumike na kukutumia mbele za Mungu. Unapojibiwa usiridhike bali jibu likupe nguvu ya kuendelea kuomba zaidi. Chochote kilicho chako ambacho umekipata kwa maombi, kisimamie kwa maombi kisipotee. Panua ulimwengu wako wa Kiroho kwa kuendeleza maombi ya kivita bila ...kunyamaza wala kunyamazishwa na kitu chochote.

    Isaya 25:10 Kwa maana mkono wa BWANA utatulia katika mlima huu, na Moabu atakanyagwa chini huko aliko, kama vile majani makavu yakanyagwavyo katika maji ya jaa. Ibilisi atakanyagwa huko chini mahali popote alipo. Panua uwanja wako wa vita katika ulimwengu wa Roho na ulimwengu wa damu na nyama. Unapofanya hivyo unazidi kusukuma adui zako wakae mbali nawe katika ulimwengu wa Roho na katika ulimwengu wa damu na nyama. Kwa kufanya hivyo unasababisha utiisho wako kuongezeka na kuwa mkubwa na adui zako wanazidi kukuogopa. Unasababisha jina lako kutukuka au kuenea kila mahali katika uhodari, ushujaa na kusababisha maadui kukuogopa wasikiapo jina lako mahali popote. Baada ya kujibiwa maombi pata nguvu tena ya kuendelea mbele na kuomba zaidi.

    #By #Mch. #Loserian #Mollel.

    See More

    report this review
  • Anynomous
    03 June 2018

    Kumpokea Yesu na kumkabidhi maisha yako ni jambo jema

    Ndugu huyu akiongozwa sala ya toba na kufanyiwa maombi ya kufunguliwa.

    report this review
  • Anynomous
    03 June 2018

    Eeh yawe tunakushukuru kwa kuwa pamoja nasi. Wew ni Mungu tunakuabudu na hakuna kama wew.

    report this review

Rate & Write Reviews